Utangulizi Wa Fasihi Andishi
Original price was: KSh 450.00.KSh 400.00Current price is: KSh 400.00.
Utangulizi wa Fasihi Andishi Utangulizi wa fasihi andishi ni kitabu kinacholenga kuwapa wanafunzi na walimu wao msingi thabiti wa fasihi andishi. Kimsingi, kinalenga kumuelimisha msomaji kuhusu vigezo mbalimbali vya uchambuzi
wa fasihi andishi. Kinaangazia kwa kina tanzu za fasihi andishi. Aidha, kinadadavua tamathali za usemi zinazotumika katika fasihi andishi. Pia, kimechanganua mitindo mbalimbali ya maswali yanayoulizwa katika mijarabu/mitihani. Kitabu hiki ni muhimu sana kwa walimu, wanafunzi na wote wanaoienzi fasihi andishi.
Anne Wasike ni mwandishi wa fasihi ya Kiswahili.
Description
Makosa ya Kawaida katika Kiswahili ni mkusanyiko wa takribani maneno 2000 yanayotumiwa visivyo. Mapungufu hutokea kwa kutojua, kusahau na mazoea. Ukoseaji katika kuandika au kupiga chapa husababisha mategu. Kasoro hizo hukanganya maana ya maneno, sentensi au aya. Kimsingi, makosa huzuia uelewaji wa Kiswahili ongezi na andishi. Taksiri hizo hulemaza na kuchafua lugha sanifu.
Madhumuni ya kitabu hiki ni kusahihisha aina za makosa ili kizazi cha elimu kisiyatumie kwa namna ghalati.
Waandishi wa kitabu hiki, Timothy Omusikoyo Sumba na Sussy Nandama Sumbi ni wataalamu wa Kiswahili. Timothy Omusikoyo Sumba ni mhariri na mwandishi maarufu wa vitabu vya Kiswahili. Awali alikuwa mwalimu na mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Howard nchini Marekani. Sussy Nandama Sumbi ni mhariri na mwandishi hodari wa vitabu vya Kiswahili. Yeye ni mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya.
Reviews
There are no reviews yet.