Familia ya Bwana Heri ilitikiswa alipopoteza kazi. Pakawa na mabadiliko ya makazi, shule na marafiki. Afya ya akili ya Pili na Bela iliathirika kwa sababu ya msongo wa mawazo. Jamii nyingi hupuuza Afya ya Akili.
Katika CBE, afya ya akili imetiliwa maanani. Ni suala la msingi katika karne ya ishirini na moja. Pili anaanzisha klabu ya Dawa ya Moyoni na wanafunzi hujadili jinsi ya kudhibiti msongo wa mawazo. Wanafunzi huongozwa na kauli:
"Afya ya Akili ni kama pumzi; ukiifungia mapafuni, unaumia zaidi."